Makala ya 34 ya dimba la AFCON mwaka 2023 yaliyocheleweshwa kutoka mwaka jana, yataanza rasmi Jumamosi usiku kwa mchuano kati ya wenyeji Ivory Coast dhidi ya Guinea Bissau.
Kundi A:
Ivory Coast
Nigeria
Guinea Bissau
Equitorial Guinea
Kundi B
Misri
Ghana
Cape Verde
Musumbiji
Kundi C
Senegal
Cameroon
Gambia
Guinea
Kundi D
Algeria
Mauritania
Burkina Faso
Angola
Kundi E
Tunisia
South Africa
Mali
Namibia
Kundi F
Morocco
Tanzania
Zambia
DR Congo
Kwa mara ya tatu timu 24 zinashiriki katika patashika hiyo kati ya Januari 13 na Februari 11 huku jumla ya mikwagurano 52 ikisakatwa.
Viwanja sita vilivyo katika miji mitano vitaandaa mechi hizo huku sherehe za ufunguzi na ,mechi ya ufunguzi na fainali zikiratibiwa kuandaliwa katika uwanja wa Allasana Qatara unaoselehi mashabiki 60,000.
Sherehe za kufungua mashindano zitaanza rasmi saa tatu usiku .
Baadhi ya wachezaji nyota katika kipute cha mwaka huu ni Sadio Mane wa Senegal,Mohammed Salah wa Misri,Victior Osimhen wa Nigeria,Hakim Ziyech wa Morocco,Ryad Mahrez wa Algeria,Mohammed Kudus wa Ghana .