Home Habari Kuu Maktaba ya Meli yawasili Mombasa

Maktaba ya Meli yawasili Mombasa

0
MV Logos Hope, Picha - Hisani

Wakenya ambao wanapenda kusoma vitabu wana kila sababu ya kutabasamu kufuatia kutia nanga kwa meli iliyo maktaba katika Bandari ya Mombasa na ambayo itasalia huko kwa siku 45.

Meli hiyo kwa jina MV Logos Hope ambayo ndiyo maktaba kubwa zaidi inayoelea majini, iliwasili Mombasa miaka 15 baada ya meli sawia kwa jina MV Duolos kuwasili humo.

Logos Hope ya urefu wa mita 132 inayoendeshwa na shirika lisilo la kibiashara la GBA Ships la Ujerumani ilifika Mombasa Jumanne Agosti 22, 2023 ikiwa na vitabu zaidi ya 5000 na wahudumu 350, raia wa nchi 70 tofauti.

Kando na eneo la maktaba, meli hiyo ina mkahawa wa kimataifa, eneo la wageni na eneo la kukaribishia wageni.

Ujio wa MV Logos Hope nchini Kenya umefanikishwa na ushirikiano kati ya mamlaka ya kusimamia bandari nchini KPA, kampuni ya Inchcape, serikali ya kaunti ya Mombasa na bodi ya utalii ya Kenya.

Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya kusimamia bandari nchini KPA William Ruto, amekaribisha ujio wa meli hiyo akiutaja kuwa muhimu sio tu kwa bandari ya Mombasa bali pia kwa nchi kwa jumla

Wageni wa umri wa kati ya miaka 3 na 60 watakubaliwa kuingia kwenye meli hiyo baada ya kulipa abda ili kunufaika na yaliyomo.