Home Habari Kuu Makatibu waandamizi 50 walioteuliwa na Rais kufahamu hatima yao leo

Makatibu waandamizi 50 walioteuliwa na Rais kufahamu hatima yao leo

0

Makatibu waandamizi 50 ambao waliteuliwa na Rais William Ruto mwezi Machi mwaka huu, watafahamu hatima yao leo Jumatatu Juni 3, 2023.

Hii ni pale mahakama ya juu itakapotoa uamuzi wake kwenye swala hilo.

Taarifa kutoka kwa idara ya mahakama inaashiria kwamba uamuzi huo utatolewa saa nane unusu mchana.

Awali, mahakama ilikuwa imeomba wanahabari kutayarisha vifaa vyao ili kupeperusha matukio ya kikao hicho kuanzia saa mbili unusu asubuhi lakini mabadiliko yakafanywa na sasa kikao hicho kitafanyika kuanzia saa nane na nusu mchana.

Mahakama imeelezea pia kwamba kikao hicho kitapeperushwa mubashara kwenye vyombo vya habari kwa sababu umma ungependa kufahamu.

Rais Ruto aliteua makatibu waandamizi 50 ilhali nafasi zilizokuwa zimetangazwa na tume ya utumishi wa umma zilikuwa 23 pekee.

Waliowasilisha kesi mahakamani wanadai kwamba nafasi nyingine 27 ziliundwa kinyume cha katiba. Bunge halikuwasaili makatibu hao waandamizi kwa sababu halikuwa na mamlaka ya kuwasaili.

Mahakama ya juu ilizuia makatibu hao waandamizi wasianze kazi Machi 24 hadi pale ambapo kesi iliyowasilishwa na chama cha mawakili, LSK na Katiba Institute itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Jaji Hedwig Ong’undi aliwazuia pia wasipokee mshahara na marupurupu hadi kesi hiyo iamuliwe.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here