Home Kimataifa Makala ya 33 ya Michezo ya Olimpiki kufunguliwa rasmi leo

Makala ya 33 ya Michezo ya Olimpiki kufunguliwa rasmi leo

Washiriki wa kenya ni pamoja wanariadha 54,wachezaji raga 12,wachezaji voliboli 12,waogeleaji wawili,mchezaji fencing mmoja na mchezaji Judo mmoja.

0
kra

Makala ya 33 ya Michezo ya Olimpiki yatafunguliwa rasmi leo Ijumaa usiku jijini Paris nchini Ufaransa, yakileta pamoja zaidi ya mataifa 200.

Kinyume cha makala yaliyopita 32, sherehe za ufunguzi kwa mara ya kwanza mwaka huu hazitaandaliwa ndani ya uwanja bali kwenye Mto Seine katikati ya Paris.

kra

Baadhi ya wasanii maarufu watakaotumbuiza katika sherehe hizo ni Celine Dion, Snoop Dog, Lady Gaga na Aya Nakamura.

Wasanii Lady Gaga na Celine Dion baadhi ya watakaotumbuiza Olimpiki

Wachezaji kutoka mataifa yote 200 watahudhuria, huku wachezaji wawili kila taifa wakitumia mashua zitakazopiga gwaride umbali wa kilomita sita.

Kenya inajivunia kuwa taifa lenye ufanisi mkubwa katika michezo hiyo ya kila baada ya miaka minne barani Afrika, ikizoa jumla ya dhahabu 35,fedha 42 na shaba 36.

Michezo hiyo itaandaliwa katika kipindi cha siku 19 kuanzia Julai 24 hadi Agosti 11.

Jumla ya mashindano 329 yataandaliwa yakijumuisha mataifa 200 pamoja na timu ya Olimpiki.

Kijiji cha Olimpiki wanakoishi wanamichezo na maafisa wao

Fani 32 zinashirikishwa katika makala ya mwaka huu ikiwemo michezo 4 mipya.

Wanamichezo wapatao 10,500 wanashiriki, Kenya ikiwa na timu ya wachezaji 81.

Mto Seine kutakapoandaliwa sherehe za ufunguzi wa Olimpiki

Washiriki wa Kenya ni pamoja wanariadha 54, wachezaji raga 12,wachezaji voliboli 12, waogeleaji wawili, mchezaji wa mchezo aina ya fencing mmoja na mchezaji Judo mmoja.

Runinga ya taifa KBC Channel 1 na runinga ya Y254 zitarusha mubashara michezo hiyo.