Home Habari Kuu Makahama ya Nairobi yasitisha kwa muda kutumwa kwa polisi Haiti

Makahama ya Nairobi yasitisha kwa muda kutumwa kwa polisi Haiti

0

Makahama moja katika kaunti ya Nairobi imesitisha kwa muda mpango wa kutuma maafisa wa polisi wa Kenya nchini Haiti kudumisha amani.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tayari limeridhia mpango huo, ambapo Kenya imepangiwa kuongoza kikosi cha kimataifa kitakachotumwa katika nchi hiyo ya Carribean.

Jaji Chacha Mwita amesitisha mpango wa serikali ya Kenya kuwatuma maafisa hao hadi kesi iliyowasilishwa na chama cha Thirdway Alliance itakaposikizwa.

Maelekezo kuhusu kesi hiyo yanatarajiwa kutolewa Oktoba 24.

Kiongozi wa chama cha Thirdway Alliance Dkt. Ekuru Aukot alimshtaki Rais William Ruto na viongozi wakuu serikalini Ijumaa iliyopita kwa kupanga kuwatuma maafisa 1,000 nchini Haiti kinyume cha sheria.

Waziri wa Usalama wa Kitaifa Kithure Kindiki awali aliashiria kuwa maafisa hao watatumwa nchini Haiti baada ya Bunge la Taifa kuridhia mpango huo kwa mujibu wa katiba.

Website | + posts