Home Kaunti Maji katika ziwa Olbolosat yaongezeka kwa asilimia 40

Maji katika ziwa Olbolosat yaongezeka kwa asilimia 40

Ziwa hilo katika muda wa miezi tano iliyopita, lilikuwa na kiwango kidogo cha maji cha chini ya asilimia 10.

0
Ziwa Olbolosat kaunti ya Nyandarua.
kra

Msimu wa mvua unaoshuhudiwa katika kaunti ya Nyandarua, umesababisha maji katika ziwa Olbolosat kuongezeka kwa asilimia 40.

Ziwa hilo katika muda wa miezi tano iliyopita, lilikuwa na kiwango kidogo cha maji cha chini ya asilimia 10.

kra

Ukosefu huo wa maji katika ziwa hilo hapo awali, ulisababisha mgogoro kati ya jamii za eneo hilo, wafugaji wa kuhamahama na kati ya binadamu na wanyama,

Hata hivyo, ili kuhakikisha jamii ya eneo hilo linanufaika na shughuli za utalii, wakazi wametoa wito kwa serikali kujenga barabara inayoelekea katika ziwa hilo.

Wakati huo huo, wakazi hao walihoji fedha zinazokusanywa kutoka Thompson Falls kupitia watalii wa hapa nchini na wale wa kigeni, walizosema zinapaswa kutumiwa kuhifadhi ziwa Olbolosat ambalo hupeleka maji yake  ndani ya Thomson Falls.

Aidha walitoa wito kwa waziri wa utalii Rebecca Miano kuimarisha shughuli za utalii katika ziwa hilo, ili kufikia hadhi ya vivutio vingine vya utalii katika eneo la kati mwa nchi.

Ziwa hilo hupata maji yake kutoka chemichemi za chini ya ardhi, mvua na mito kutoka maeneo ya Oljororok.

Kaunti tano hunufaika kutoka kwa ziwa Ol’bolosat ambazo ni pamoja na Laikipia, Isiolo,Samburu, Garissa na Wajir.

Website | + posts
Lydia Mwangi
+ posts