Home Kaunti Majambazi wavamia shule huko Kirinyaga

Majambazi wavamia shule huko Kirinyaga

0
Wanafunzi wa shule ya upili ya Kiaga.

Ijumaa Septemba 1, 2023,  usiku, majambazi walivamia shule ya kutwa ya mseto na ya upili ya Kiaga huko Kirinyaga na maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi.

Majambazi hao wanne waliwashika mateka walinzi wa shule hiyo kabla ya kuvunja afisi ya mwalimu mkuu na kuiba viwambo viwili vya runinga, tarakilishi, simu na kamera za CCTV.

Video iliyonakiliwa na kamera hizo inaonyesha majambazi hao wakirandaranda shuleni humo baada ya kufunga walinzi kwa kamba.

Maafisa wa upelelezi kutoka kaunti ndogo ya Kirinyaga ya kati waliozuru eneo la tukio wanasema walinzi hao walipatwa wakiwa wamefungwa kwa kamba wakasaidiwa na kupelekwa hospitalini kwa matibabu.

Mmoja wa walinzi hao alisema kwamba wezi hao walikuwa wamejihami kwa bunduki na panga.

Website | + posts