Home Habari Kuu Majambazi wavamia kambi ya Kakuma na kumuua mtu mmoja

Majambazi wavamia kambi ya Kakuma na kumuua mtu mmoja

Idadi isiyojulikana ya majambazi waliojihami kwa bunduki wamevamia kambi ya wakimbizi ya Kakuma siku ya Ijumaa na kumuua raia mmoja wa Sudan Kusini .

0

Idadi isiyojulikana ya majambazi waliojihami kwa bunduki wamevamia kambi ya wakimbizi ya Kakuma siku ya Ijumaa na kumuua raia mmoja wa Sudan Kusini .

Shambulizi hilo limetokea katika kijiji cha Kalobeyei ndani ya kambi ya wakimbizi ya Kakuma .

Majambazi hao walikuwa wamejihami kwa bunduki aina ya AK 47 waliwapiga risasi watu wengine watatu huku marehemu akipigwa risasi ya kichwani alipokuwa akijaribu kutorokea kichakani.

Polisi wamesema wanaendelea kuchunguza shambulizi hilo na mauaji hayo.