Home Habari Kuu Majaji watakiwa kujiepusha na ufisadi

Majaji watakiwa kujiepusha na ufisadi

Bila uadilifu, alidokeza, uaminifu wa Mahakama, pamoja na taasisi zote za umma, ungetiliwa shaka vikali.

0
Rais William Ruto.
kiico

Rais Ruto aliwataka majaji hao kukataa aina yoyote ya ufisadi na kuwatumikia Wakenya kwa uadilifu na weledi.

“Nawahimiza mujitolee katika kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na weledi, na kukataa rushwa kwa kila dalili zake,” alisema.

Bila uadilifu, alidokeza, uaminifu wa Mahakama, pamoja na taasisi zote za umma, ungetiliwa shaka vikali.

“Ufisadi, hata kidokezo kidogo zaidi, uhatarisha mamlaka na ufanisi wa mahakama zetu kwa njia isiyoweza kutenduliwa,” alisema Rais.

Ili kuwapa Wakenya ahadi kamili ya Katiba, Rais Ruto aliwataka majaji kusalia hai kwa Vifungu 10 na 159 pamoja na kiapo chao cha kuhudumu.

“Kujitolea kwenyu kwa mamlaka na ahadi hizi, na kujitolea kwenyu kuwatumikia watu wa Kenya kwa bidii, na kuwatendea haki – bila woga, upendeleo, mapenzi, nia mbaya, chuki au ushawishi wowote wa kisiasa, kidini au mwingine – kuleta tofauti kati ya maendeleo na kushindwa, uhuru na dhuluma, na ustawi na ufukara kwa watu wa taifa letu pendwa,” akasema Dkt Ruto.

kiico