Home Habari Kuu Mahakama yasitisha ulipaji karo kupitia eCitizen

Mahakama yasitisha ulipaji karo kupitia eCitizen

Jaji Chacha Mwita alisema baada ya kusoma maombi ya kesi hiyo, yaliowasilishwa kwake, aliridhika  kwamba swala muhimu lilikuwa limeangaziwa.

Mahakama kuu imetoa amri ya kusitisha  kwa muda malipo ya karo ya shule za upili za umma kupitia tovuti ya serikali  ya eCitizen.

Jaji Chacha Mwita alisema baada ya kusoma maombi ya kesi hiyo, yaliowasilishwa kwake, aliridhika  kwamba swala muhimu lilikuwa limeangaziwa.

Kwenye barua ilioandikwa tarehe  31 mwezi Januari mwaka huu, katibu wa elimu ya msingi  Belio Kipsang, aliwaaagiza wazazi kulipa karo kupitia tovuti ya serikali ya eCitizen.

Jaji Mwita alisema maagizo zaidi kuhusiana na kesi hiyo yatatolewa tarehe 13 mwezi  Februari mwaka huu.

Serikali imekuwa kwenye harakati ya kuweka huduma zote kwenye tovuti ya  eCitizen, ili kuimarisha utoaji huduma.

Rais William Ruto alipowahutubia wakenya wanaoishi nchini Japan siku ya Jumanne, alisema sera hiyo mpya inayohitaji karo ya shule kulipwa kupitia tovuti ya eCitizen, inalenga kuondolea mbali malipo ambayo sio halali yanayotozwa na baadhi ya shule.

Alisema serikali imejitolea kuhakikisha inakamilisha uhamisho wa mifumo ya malipo kwa mfumo wa kidijitali.

Website | + posts
Radio Taifa
+ posts