Home Habari Kuu Mahakama yasitisha agizo la Kindiki kuhusu kufungwa kwa baa

Mahakama yasitisha agizo la Kindiki kuhusu kufungwa kwa baa

0

Mahakama kuu jijini Kisumu imesitisha agizo la Waziri wa Usalama wa ndani Kithure Kindiki ya kifungwa kwa baa katika harakati za kukabili uuzaji wa pombe haramu.

Uamuzi huo umetolewa na mahakama hiyo wakati kesi kuhusiana na agizo hilo inasubiri kusikilizwa.

Wamiliki wa baa Kisumu walikuwa wamewasilisha kesi wakipinga agizo hilo la waziri Kindiki.

Profesa Kindiki alitoa agizo la kufungwa kwa baa zote zinazohudumu katika maeneo ya makazi na shule mnamo Machi 6, 2024.

Aidha aliagiza baa zinazomilikiwa na watumishi wa umma zifungwe.

Serikali iliagiza kuwa maafisa wa umma wanaomiliki au kuendesha baa wazifunge au wajiuzulu.

Alphas Lagat
+ posts