Home Habari Kuu Mahakama yasimamisha utekelezaji wa bima mpya ya afya

Mahakama yasimamisha utekelezaji wa bima mpya ya afya

0

Jaji wa mahakama kuu E.C Mwita amesimamisha utekelezaji wa bima mpya ya afya inayochukua mahala pa bima ya kitaifa ya matibabu NHIF.

Hatua hii inafuatia kesi iliyowekwa katika mahakama hiyo na mkenya kwa jina Aura Joseph Enock dhidi ya wizara ya afya, Novemba 24, 2023.

Jaji Mwita ameelekeza kwamba washtakiwa wa kesi hiyo wapatiwe stakabadhi za kesi mara moja na wawasilishe majibu yao mahakamani katika muda wa siku 7.

Mlalamishi naye ana muda wa siku saba kuwasilisha hati ya kiapo ya ziada iwapo itahitajika na isizidi kurasa 10.

Mawasilisho ya washtakiwa nayo yanatakiwa kuwa chini ya kurasa 10.

Kutokana na kesi hii, wizara ya afya na washirika wake imetakiwa kutotekeleza sheria tatu za sekta ya afya zinazolenga bima ya afya ambazo ni sheria ya bima ya afya ya jamii ya mwaka 2023,
Sheria ya afya ya msingi ya mwaka 2023 na sheria ya afya kidijitali ya mwaka 2023 hadi Februari 7, 2024.

Arifa ya jaji Mwita imetolewa leo Novemba 27, 2023.