Home Kimataifa Mahakama yasimamisha jopokazi la kuchunguza deni la taifa

Mahakama yasimamisha jopokazi la kuchunguza deni la taifa

Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya chama cha mawakili nchini LSK, kusema jopokazi hilo lilibuniwa kinyume cha sheria.

0
Mahakama Kuu yasimamisha agizo la kaimu Inspekta Jenerali wa polisi la kupiga marufuku maandamano jijini Nairobi.
kra

Mahakama kuu imesimamisha jopokazi la kirais kuhusu ukaguzi wa deni la taifa, kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi iliyowasilishwa.

Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya chama cha mawakili nchini LSK, kusema jopokazi hilo lilibuniwa kinyume cha sheria.

kra

Huku akisema swala hilo ni la dharura, Jaji wa Mahakama Kuu Lawrence Mugambi, aliwazuia wanachama wa jopokazi hilo dhidi ya kutekeleza majukumu yao hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Aidha Jaji huyo pia aliagiza kwamba ilani za kesi hiyo ziwasilishwe kwa kwa mwanasheria mkuu na washtakiwa wengine katika muda wa siku tatu zijazo, huku majibu yakitarajiwa katika muda wa siku saba zijazo.

Kesi hiyo inayopinga kubuniwa kwa jopokazi hilo, iliyowasilishwa na Eunice Ng’ang’a, Dkt. Magare Gikenyi na Eliud Matindi, ilisema kuambatana na katiba jukumu la ukaguzi wa deni la taifa ni la Mkaguzi Mkuu wa hesabu za umma,  na hivyo jopo kazi hilo litakuwa likifuja rasilmali za umma huku miito ikitolewa ya kupunguza matumizi ya pesa za serikali.

Rais wa chama cha mawakili nchini Faith Odhiambo ambaye alichaguliwa katika jopokazi hilo, alisema hatachukua wadhifa huo, akitaja jopokazi hilo kuwa si halali.

Ijumaa iliyopita Rais Ruto alibuni Jopokazi la kufanya uchunguzi wa deni la taifa, huku akimteua Nancy onyango kuwa mwenyekiti wake.

Wengine walioteuliwa katika jopokazi hilo ni pamoja na Prof. Luis G. Franceschi, mwenyekiti wa ICPAK Phillip Kaikai, Rais wa chama cha wahandisi nchini Shammah Kiteme, na mtaalam wa sera na uongozi Vincent Kimosop.

Jopokazi hilo lilibuniwa kupitia gazeti rasmi la serikali la Julai 5, 2024, muda mfupi baada ya rais kuhutubia taifa katika Ikulu ya Rais, ambapo alitangaza mikakati ya kupunguza matumizi ya serikali kufuatia kuondolewa kwa Mswada wa Fedha 2024.

Website | + posts