Home Habari Kuu Mahakama yaondoa marufuku ya Seneta Orwoba

Mahakama yaondoa marufuku ya Seneta Orwoba

0

Mahakama kuu ya Nairobi imebatilisha uamuzi wa bunge la seneti kumpiga marufuku seneta mteule Gloria Orwoba kwa miezi sita.

Kulingana na taarifa hiyo mahakama kuu imeondoa marufuku hiyo kwa muda kusubiri kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi iliyowasilishwa na Seneta huyo,ambayo itatajwa tarehe 25 mwezi ujao.

Seneta Orwoba alienda mahakamani wiki jana akisema marufuku dhidi yake ilikuwa ukiukaji wa haki zake .

Bunge la Seneti pia lilimzuia Orwoba kukanyaga ndani ya majengo ya bunge kwa miezi sita ijayo ya kikao cha pili cha bunge la 13.

Adhabu ya Orwoba ilitokana na matamshi yake ya kuwashutumu baadhi ya viongozi wanaume wa bunge hilo kwa kuwadhulumu kimapenzi maseneta wa kike .