Home Kimataifa Mahakama yamzuia Zuma kuwania ubunge

Mahakama yamzuia Zuma kuwania ubunge

0

Mahakama moja Afrika Kusini, imemuzuia Rais wa zamani wa taifa hilo Jacob Zuma kuwania kiti cha bunge Kwa sababu ya kifungo Cha miezi 15 alichohukumiwa mwaka wa 2021.

Zuma alihukumiwa kifungo hicho Kwa kupuuza amri ya mahakama ya kumtaka afike mbele ya tume iliyokuwa ikichunguza madai ya ufisadi dhidi yake.

Kwa mujibu wa mahakama hiyo, kifungo Cha zaidi ya miezi 12 na kisicho ruhusa faini humzuilia yeyote kumiliki afisi ya umma Kwa miaka mitano.

Hata hivyo, chama chake kipya Cha uMkhonto weSizwe kimekiri kuwa hatua hiyo haitalemaza harakati za chama hicho kwenye uchaguzi wa wiki ijayo.

Zuma aliongoza taifa hilo tangu mwaka wa 2009 na kujiuzulu mwaka wa 2018 kutokana na shutuma za ufisadi.