Home Taifa Mahakama ya upeo yamaliza kusikiliza rufaa ya sheria ya fedha ya mwaka...

Mahakama ya upeo yamaliza kusikiliza rufaa ya sheria ya fedha ya mwaka 2023

0
Jaji Mkuu na Rais wa mahakama ya upeo Martha Koome
kra

Mahakama ya upeo leo imehitimisha kusikiliza Ombi lililotolewa na asasi mbali mbali za serikali ikiwa ni pamoja na Bunge, afisi ya Mwanasheria Mkuu na waziri wa fedha wanataka Sheria hiyo ya Fedha ya mwaka 2023 irejeshwe.

Wanaopinga kurejeshwa kwa Sheria hiyo wakiongozwa na Seneta wa Busia Okiya Omutata walipinga kesi hiyo huku majaji wakiongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome pia wakitaka ufafanuzi kuhusu masuala muhimu ya rufaa hiyo.

kra

Miongoni mwa masuala yaliyoibuliwa wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo ni swali la iwapo kumekuwa na ushirikishi wa kutosha wa wananchi na iwapo kulikuwa na lazima ya maelewano kati ya Bunge la Kitaifa na Seneti kuhusu marekebisho yaliyofanywa na Bunge lolote bila kuhusika na lingine kabla ya kupitishwa kwa Sheria hiyo.

Rufaa hiyo imewasilishwa na Bunge, Spika wa Bunge, Mwanasheria Mkuu, waziri wa fedha na mamlaka ya kukusanya ushuru KRA, dhidi ya hukumu iliyotokana na ombi la walalamishi 53 wakiongozwa na Seneta wa Busia Okiya Omutata.

Wakili wa Bunge Issa Mansour alisisitiza msimamo kwamba kumekuwa na ushirikishi wa umma wa kutosha na kwamba kuna njia wazi kwa wananchi kufuatilia maendeleo ya mchakato wa kutunga sheria ikiwa ni pamoja na kufuatilia maoni waliyotoa wakati wa hatua ya ushirikishi wa umma.

“Kituo cha televisheni cha Bunge kiko wazi kwa Umma na shughuli zote za Bunge ziko wazi kwa Umma. Zaidi ya hayo, Bunge la Kitaifa lina akaunti za mitandao ya kijamii ambapo shughuli zake zote huwekwa, ambazo ni ukurasa wa Facebook wa Bunge la Kenya na akaunti ya mtandao wa X. Bunge pia lina eneo la umma lililo wazi kwa raia yeyote kufuatilia vikao vya Bunge.” alisema Mansour.

Profesa Githu Muigai ambaye ni wakili wa mwanasheria mkuu na waziri wa fedha alionya dhidi ya kuzingatia hukumu ya mahakama ya rufani akisema itakuwa sawa na kulemaza shughuli za Serikali.

“Mahakama inapaswa kuepuka maamuzi makali ambayo yanatawala uthabiti wa serikali ilivyofanya mhakama Kuu. Kupokonya serikali fedha sio jambo jepesi.” alisema Muigai.

Mahakama itatoa hukumu baadaye.

Website | + posts