Home Michezo Mahakama ya Ulaya yamuunga mkono Semenya katika vita dhidi ya ubaguzi

Mahakama ya Ulaya yamuunga mkono Semenya katika vita dhidi ya ubaguzi

0

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu (ECHR) imekubali rufaa ya mwanariadha wa Afrika Kusini, Caster Semenya, dhidi ya shirika la kimataifa linalosimamia riadha.

Mahakama ilisema amekuwa akibaguliwa kwa sababu ya sharti kwamba apunguze viwango vyake vya juu vya testosterone asilia ili kushindana katika mbio za wanawake.

Semenya ni bingwa wa Olimpiki mara mbili katika mashindano ya mita 800 – lakini kukataa kwake kupunguza viwango vya homoni yake kimatibabu kulisababisha kuzuiwa kushiriki mashindano hayo tangu mwaka 2019.

Alidai kuwa sheria zilizotekelezwa na Riadha za Ulimwengu zilikiuka haki yake ya kushiriki kwa uhuru katika michezo ya wanawake, licha ya kutambuliwa kisheria kama mwanamke wakati wa kuzaliwa, na kujitambulisha kama mwanamke maisha yake yote.

feedback@kbc.co.ke | Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here