Home Kimataifa Mahakama ya Kikatiba Uganda yakataa kuharamisha sheria zinazopinga ushoga

Mahakama ya Kikatiba Uganda yakataa kuharamisha sheria zinazopinga ushoga

0

Mahakama ya Kikatiba nchini Uganda siku ya Jumatano ilikataa kuharamisha sheria mpya ya mwaka 2023 inayopinga ushoga na usagaji.

Hata hivyo, majaji watano wa mahakama hiyo waliondoa vipengee kadhaa katika sheria hiyo wakivitaja kuwa kinyume cha dini na vinavyokiuka haki ya watu kuwa na afya bora.

Mahakama hiyo imetenga Disemba 11 mwaka huu kuwa siku ya kusikiza kesi zinazopinga sheria za kuharamisha ushoga na usagaji zilizoidhinishwa mwaka 2023.

Sheria hizo ziliwasilishwa na wanaharakati.

Rais Yoweri Museveni ameapa kutokubali tamaduni za nchi za Magharibi kama vile na ushoga na usagaji kutamalaki nchini humo, na msimamo wake huo umekuwa chanzo cha nchi hiyo kuwekewa vikwazo kadha wa kadha.

Hata hivyo, anashikilia kuwa vikwazo hivyo havitabadili msimamo wake.

Website | + posts