Home Kimataifa Mahakama Kuu yaongeza muda wa kutokamatwa kwa Wanjigi

Mahakama Kuu yaongeza muda wa kutokamatwa kwa Wanjigi

0
kra

Mahakama Kuu ya Kenya imeongeza muda wa agizo la kutokamatwa kwa mfanyabiashara Jimi Wanjigi.

Kwenye uamuzi wake, Jaji Bahati Mwamuye ameongeza muda huo kuzuia kukamatwa kwa Wanjigi hadi Septemba 19.

kra

Hata hivyo, mahakama haijatoa vikwazo dhidi ya Wanjigi kufunguliwa mashtaka mapya.

Kesi hiyo itatajwa tena Septemba 19 mwaka huu.

Wanjigi amekwaruzana na maafisa wa polisi katika siku za hivi karibuni kwa tuhuma kuwa amekuwa akifadhili maandamano ya vijana wa Gen Z, madai ambayo amekanusha vikali.

Siku chache zilizopita, maafisa wa polisi walivamia nyumbani kwake wakitaka kumkamata ila hawakumpata.

Ni hatua iliyomlazimu Wanjigi kukimbilia mamlaka na kupata agizo la kuzuia maafisa wa polisi kumkamata.

Wanjigi amekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Kenya Kwanza anaoutuhumu kwa kuyumbisha uchumi wa nchi.

Website | + posts