Mahakama Kuu imeondoa agizo la kuzuia utekelezaji wa matumizi ya vitambulisho vipya maarufu kama Maisha Namba.
Mahakama hiyo imemkosoa Jaji Lawrence Mugambi aliyetoa agizo la kusimamisha utekelezaji wa vitambulisho hivyo vipya ikisema hakuzingatia matakwa ya umma.
Katibu wa Idara ya Uhamiaji Julius Bitok amesema kuwa tayari mchakato wa uchapishaji vitambulisho 1,215,095 ulikwama mwezi Julai kutokana na agizo hilo.
Vitambulisho hivyo vipya vitachukua nafasi ya vile vya sasa, huku vikitumika kupata huduma kadhaa za serikali kinyume na ilivyo kwa sasa.