Home Habari Kuu Mageuzi katika sekta ya kahawa yanaendelea, asema Rigathi Gachagua

Mageuzi katika sekta ya kahawa yanaendelea, asema Rigathi Gachagua

Gachagua aliwataka wakulima wa kahawa kuwa na subira na serikali.

0

Naibu wa Rais Rigathi Gachagua amesema serikali haitazuiwa katika harakati za kuboresha maslahi ya wakulima.

Akizungumza katika mkutano na wadau wa sekta ndogo ya kahawa nchini, Gachagua alisema, serikali haitapumzika hadi wakiritimba wote waangamizwe.

Alidokeza kuwa serikali haitatishwa na shinikizo kutoka kwa makundi ya wakiritimba yanayojaribu kuteka nyara sekta ya kahawa ili kuendelea kuwapunja wakulima.

Alielezea kuwa Rais William Ruto yuko makini na mageuzi yanayoendelea katika sekta ya kilimo, ikiwemo sekta ndogo ya kahawa huku akiwataka wakulima wa kahawa kuwa na subira na serikali.

Mkutano huo ulioandaliwa katika afisi ya Naibu Rais iliyoko jumba la Harambee Annex Jijini Nairobi, ulihudhuriwa pia na Mkuu wa Utumishi wa Umma  Felix Koskei, Waziri wa Vyama vya Ushirika Simon Chelugui na Katibu katika Afisi ya Naibu Rais Julius Korir miongoni mwa wengine.

Kwa upande wake, Koskei alisema wakati umewadia wa kuyafurusha makundi yote ya wakiritimba yanayowalaghai wakulima na kuwaacha wakiteseka.

Naye Waziri Chelugui alisema serikali iko tayari kutafuta mbinu mbadala kuwakinga wakulima.

Website | + posts