Home Kimataifa Magavana watakiwa kutoa kipaumbele kwa afya ya msingi

Magavana watakiwa kutoa kipaumbele kwa afya ya msingi

0
kra

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha amesisitiza haja ya kutoa huduma msingi za afya, PHC ili kufanikisha upatikanaji wa afya kwa wote, UHC kote nchini. 

Ametoa wito kwa magavana kutoa kipaumbele kwa utoaji huduma msingi za afya, hatua anayosema itasaidia katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma za bei nafuu za matibabu kwa Wakenya wote.

kra

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mpango wa UHC Mashujaa katika uwanja wa Kapkatet kaunti ya Kericho, Waziri Nakhumicha alielezea uwezakano wa utoaji huduma msingi za afya kubadilisha mfumo wa afya nchini na kutoa wito wa kuwepo ushirikiano baina ya kaunti zote 47 nchini.

Hafla ya ufunguzi wa mpango wa UHC Mashujaa iliongozwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua, ikiwa ishara ya hatua muhimu zinazopigwa na serikali katika azima ya Kenya kuhakikisha upatikanaji wa afya kwa wote.

Siku ya Mashujaa itaadhimishwa Ijumaa wiki hii huku kaulimbiu ya sherehe za mwaka huu ikiwa “Upatikanaji wa Afya kwa Wote.”

Website | + posts