Home AFCON 2023 Mafarao wa Misri na Ghana wahaha AFCON

Mafarao wa Misri na Ghana wahaha AFCON

0

Misri na Ghana wamejipata kwenye njia panda katika hekaheka za kuwania kombe la AFCON, baada ya kuambulia sare ya magoli mawili katika mechi ya kundi B iliyosakatwa jana Alhamisi usiku nchini Ivory Coast.

Mohamed Kudus alipachika magoli yote ya Black Stars ya Ghana huku Omar Marmoush na Mustafa Mohamed, wakibusu nyavu upande wa mafarao.

Timu zote zinasalia bila ushindi Ghana ikiwa na alama moja huku Misri wakizoa pointi 2.

Misri ni sharti waibwage Cape Verde katika mkwangurano wa mwisho Jumatatu ijayo, huku Ghana wakiwa hawana budi kuwashinda Msumbiji ili kufuzi kwa raundi ya 16 bora.