Home Kimataifa Maelfu ya watu wahofiwa kufa baada ya mafuriko kukumba Libya

Maelfu ya watu wahofiwa kufa baada ya mafuriko kukumba Libya

0

Maelfu ya watu wanahofiwa kufa baada ya dhoruba kali kusababisha mafuriko makubwa nchini Libya.

Kiongozi wa serikali ya Libya mashariki, ambayo haitambuliki kimataifa, alisema vifo vilizidi 2,000 na maelfu hawakupatikana.

Jalel Harchaoui, mtaalamu wa Libya, aliiambia BBC kwamba idadi ya vifo inaweza kufikia watu “elfu kadhaa”.

Kimbunga Daniel kilipiga Jumapili, na kusababisha mamlaka kutangaza hali ya hatari.

Wanajeshi saba wa jeshi la Libya walitoweka wakati wa juhudi za uokoaji zinazoendelea.

Maafisa mashariki waliweka amri ya kutotoka nje, huku shule na maduka yakiamriwa kufungwa miji ya mashariki ya Benghazi, Sousse, Derna na Al-Marj yote iliathirika.

Pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vifo, Shirika la Msalaba Mwekundu la Libya limesema kuwa takriban nyumba 150 zimeharibiwa.

BBC
+ posts