Home Habari Kuu Maelfu ya wasafiri wapigwa na baridi kufuatia msongamano wa magari

Maelfu ya wasafiri wapigwa na baridi kufuatia msongamano wa magari

0

Maelfu ya wasafiri walivumilia baridi kali mapema leo Jumatatu baada ya kukesha kwenye barabara kuu ya Mombasa kufuatia msongamano wa magari uliosababishwa na ajali ya trela.

Kulingana na polisi, trela hilo lilipinduka na kufunga barabara eneo la Makindu-Kiboko, katika ajali hiyo iliyotokea jana Jumapili, saa kumi na mbili jioni.

Polisi walisema kuwa mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha eneo hilo ilitatiza shughuli ya kuondoa lori hilo ili kumaliza msongamano.

Mvua kubwa inayonyesha katika maeneo mengi nchini imetatiza usafiri baada ya kusababisha kubomoka kwa barabara.

Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen anasema serikali imechukua hatua za kuzikarabati barabara zilizoharibiwa.

Mvua hiyo imetabiriwa kuendelea hadi mwezi Januari mwakani.

Website | + posts