Mamia ya wakazi mjini Durban waliachwa bila makao baada ya moto kuteketeza nyumba zao karibu na bandari ya mjini Durban,Afrika Kusini mapema Jumapili.
Mtu mmoja anaamika kufariki kutokana na moto huo uliotokea katika mtaa wa mabanda mapema Jumapili, huku ikikisiwa huenda mili zaidi ikapatikana.
Chanzo cha moto huo ulioteketeza kila kitu hakijabainika ingawa mtu mmoja aliyeshuhudia anasema kuwa moto huo ulisababishwa na watu wawili waliokuwa wakigombana wakinywa pombe.
Kulingana na takwimu za shirika la msalaba mwendu takriban nyumba 1,000 ziliharibiwa na kuwaacha watu wapatao 3,000 bila makao.