Home Habari Kuu Maduka 120 ya kuuza vileo yafungwa eneo bunge la Starehe

Maduka 120 ya kuuza vileo yafungwa eneo bunge la Starehe

0

Zaidi ya maduka 120 ya kuuzia vileo yamefungwa na wamiliki 25 wa maduka hayo kutiwa nguvuni,  katika eneo bunge la Starehe kaunti ya Nairobi kufuatia msako uliotekelezwa na maafisa kutoka asasi mbali mbali.

Msako huo unajiri baada ya Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja kuagiza kufungwa kwa maeneo ya kuuzia pombe yaliyo karibu na vituo vya mabasi.

Juma lililopita Gavana  Sakaja aliongoza mkutano uliowaleta pampja wenyeviti wa sekta za uchukuzi wa umma na Kampuni za magari ya uchukuzi jijini Nairobi.

“Hatutakubalia utovu wa nidhamu Jijini Nairobi. Nimeagiza kufungwa kwa vituo vyote vya kuuzia pombe karibu na vituo vya matatu. Madereva na utingo wengi hutumia muda mwingi katika maduka hayo. Tumewapoteza wapendwa wetu kupitia ajali za barabarani kwa sababu ya ulevi na utumizi wa mihadarati. Tumegundua kuwa maduka hayo yanahudumu bila leseni,” alisema Gavana Sakaja.

Operesheni hiyo iliyoongozwa na afisa anayesimamia usalama na utekelezaji sheria Tony Kimani  na Judith Anyango, naibu mwenyekiti wa bodi ya udhibiti wa vileo, ililenga maduka ya kuuzia pombe katika vituo vya magari vya Muthurwa, Hakati, Accra, Latema na mzunguko wa Old nation.

Website | + posts