Madereva wa malori ya masafa marefu, wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na kuongezeka kwa visa vya ukosefu wa usalama katika barabara kuu za Kisumu – Busia na Eldoret – Malaba, ambako madereva huporwa.
Wakiongea Jumatatu mjini Malaba, madereva hao wakiongozwa na mwenyekiti wao, Peter Tanui, walidokeza kuwa majambazi hao wamekuwa wakitumiwa msongamano wa magari ambao umedumu kwa muda wa wiki mbili kupora bidhaa zinazosafirishwa.
Tanui sasa anamtaka waziri mpya wa barabara na uchukuzi kuzuru vituo vya mpakani vya Busia na Malaba na kushughulikia hali hilo .
Matamshi ya Tanui yaliungwa mkono na dereva mwenzake Hosen Adan, aliyesema kuwa wametoa makataa ya siku 14 kwa halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya- KRA, halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini Uganda – URA pamoja na ile ya Sudan Kusini kushughulikia swala hilo, la sio hivyo watasitisha uchukuzi wa bidhaa kuelekea Sudan Kusini.
Mmoja wa madereva hao alielezea jinsi alivyoporwa dola 50,000 za marekani na watu wanaoshukiwa kuwa wanajeshi wa Sudan Kusini.
Msongamano huo wa malori hayo ya masafa marefu, umefika Kanduyi, huku madereva hao wakihofia huenda ukafika Webuye.