Madaktari katika hospitali ya rufaa ya Kisii KTRH wametekeleza upasuaji wa kwanza wa uti wa mgongo.
Upasuaji huo uliofanikiwa ulichukua muda wa saa 5 na dakika 13.
Madaktari hao chini ya uongozi wa Victor Misiani mtaalamu wa masuala ya uti wa mgongo sasa wanajivunia hatua hiyo huku wakitoa wito kwa walio na matatizo kama hayo kufika hospitalini humo.