Home Habari Kuu Madaktari kurejea kazini Alhamisi baada ya kumaliza mgomo

Madaktari kurejea kazini Alhamisi baada ya kumaliza mgomo

0

Hali ya kawaida inatarajiwa kurejea katika hospitali zote za umma nchini, kaunzia siku ya Alhamisi baada ya Madaktari kutangaza kumaliza mgomo siku ya Jumatano.

Madaktari walisitisha mgomo huo  Jumatano baada ya kutia saini mwafaka wa maelewano pamoja na wizara ya afya ,hatua iliyomaliza mgomo uliokuwa umedumaza huduma za afya kwa  siku 56.

Hata hivyo mwafaka huo ulisainiwa licha ya pande zote kukosa kuafikiana kuhusu malipo ya madakatari wanagenzi wizara ya afya ikipendekeza malipo ya shilingi 70,000, huku chama cha Madaktari KMPDU kikitaka malipo ya shilingi 206,000 .

Mahakama ilikuwa imeweka Jumatano kama makataa ya madaktari na serikali kukubaliana na kuhitimisha mgomo huo.

Website | + posts