Home Habari Kuu Madaktari kufanya maandamano kote nchini Jumanne

Madaktari kufanya maandamano kote nchini Jumanne

0

Madaktari wanaogoma watafanya maandamano kote nchini Jumanne tarehe 9 Aprili,  kuishinikiza serikali itimize matakwa yao huku mgomo wa kitaifa ukitarajiwa kuingia wiki ya nne.

Mgomo huo ulianza Machi 14 mwaka huu na wameapa kuendelea kususia kazi, hadi pale matakwa yao yatakapotimizwa kikamilifu.

Mgomo huo unaendelea kusambaratisha huduma za matibabu kwenye hospitali zote za umma nchini, huku maafisa mbali mbali kama wataalamu wa maabara wakijiunga na mgomo pia.

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha, ameandaa kikao na wafanyikazi wa hospitali wasio kwenye muungano, ili kuzuia mgomo ambao unatarajiwa kaunzishwa na wahudumu hao kuanzia Jumatatu Aprili 8.

Website | + posts