Home Habari Kuu Madaktari kaunti ya Kajiado wasitisha mgomo wao

Madaktari kaunti ya Kajiado wasitisha mgomo wao

0

Chama cha madaktari na wataalam wa dawa na meno (KMPDU), kimefutilia mbali mgomo wa madaktari uliopangwa kuanza siku ya Ijumaa katika kaunti ya Kajiado, baada ya kukamilika kwa ilani ya siku saba.

Mgomo huo ulifutiliwa mbali baada ya serikali ya kaunti ya Kajiado kuafikiana na madaktari hao kuhusu maswala yaliyokuwa yameibuliwa na chama hicho cha Madaktari.

Pande hizo mbili zimekubaliana kushughulikia maswala yaliyoibuliwa, ambapo mengine ni ya kushughulikiwa kwa muda mfupi na mengine ni ya muda mrefu.

Chama cha KMPD kilikuwa kimeitisha mgomo kikilalamikia ukabila, mapendeleo, kutopandishwa cheo na kutishwa dhidi ya wanachama wake.

Maswala mengine ni pamoja na kunyimwa ruhusa ya masomo na kutowasilishwa kwa fedha wanazokatwa kwa taasisi husika.