Home Habari Kuu Macky Sall atangaza kuachia uongozi wa Senegal Aprili 2

Macky Sall atangaza kuachia uongozi wa Senegal Aprili 2

0

Rais wa Senegal Macky Sall ametangaza kuwa ataondoka uongozini tarehe 2 mwezi wa nne mwaka huu  baada ya kukamilisha muhula wa pili wa miaka mitano.

Rais Sall hata hivyo amesema hana uwezo wa kuitisha uchaguzi mkuu kabla ya Aprili 2.

Kumekuwa na taharuki huku wombijoto la kisiasa likipanda tangu Rais Sall atangaze kuahirisha uchaguzi mkuu kwa miezi 10, wengi wakihisi alikuwa na njama ya kukatalia mamlakani.

Vikao na mijadala ya kitaifa itakayoandaliwa wiki ijayo ndiyo itabaini tarehe mpya ya uchaguzi mkuu.

Rais Sall tayari amehudumu kwa kipindi cha miaka 10 inavyohitajika kisheria na haruhusiwi kuongeza muhula mwigine wa utalawa.

Senegal ni mojawapo wa mataufa yaliyokomaa kidemokrasia katika ukanda wa Afrika magharibi.

Website | + posts