Home Kimataifa Macky Sall amiminiwa sifa kwa kuridhia kustaafu

Macky Sall amiminiwa sifa kwa kuridhia kustaafu

Viongozi mbali mbali wakiwemo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki wamemtaja Sall kama kiongozi wa kutamaniwa na wengi.

1
Rais wa Senegal Macky Sall: Photo/Courtesy

Baada ya kutangaza kuwa hatawania muhula mwingine wakati wa kinyang’anyiro cha urais mwaka wa 2024, Rais wa Senegal Macky Sall ameendelea kupokea sifa kedekede kwa uamuzi wake.

Alitangaza uamuzi huo jana Jumatatu kupitia chombo cha habari cha taifa hilo la Afrika Magharibi.

Taarifa ya Macky Sall ya kutogombea tena urais nchini iliondoa wasiwasi na kutuliza joto la kisiasa baina ya upinzani na serikali ambao siku za hivi karibuni umekuwa ukiandamana kupinga uwezekano wa Macky Sall kuwania kiti hicho mwaka ujao.

Katika taarifa, Sall alisema, “Uamuzi wangu wa muda mrefu sio kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais wa Februari 25, 2024, hata kama katiba inanipa haki ya kufanya hivyo”.

Viongozi mbali mbali wakiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, UN Antonio Guterres na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, AU Moussa Faki wamemtaja Sall kama kiongozi wa kutamaniwa na wengi kwa kuweka matakwa ya wananchi wa Senegal mbele ya siasa.

Guterres kupitia mtandao wa Twitter alisema uamuzi wa Sall ni mfano muhimu sana kwa nchi yake na ulimwengu kwa ujumla.

“Nieleze kupendezwa kwangu na mwanasiasa huyu (Macky Sall) ambaye amependelea maslahi bora ya Senegal na hivyo kuhifadhi mtindo wa kidemokrasia wa Senegal ambao ni fahari ya Afrika,” Faki katika mtandao wake wa Twitter.

Katika siku za hivi karibuni, kulikuwa na tetesi kuwa rais Macky Sall angebadilisha katiba na kuwania muhula wa tatu na kuchukua mkondo wa viongozi wengine wa mataifa ya Afrika Magharibi kama Ivory Coast na Togo.

Makabiliano kati ya wafuasi wa Sonko na maafisa wa polisi yametajwa kuwa mabaya zaidi kutokea nchini humo katika siku za hivi karibuni na uamuzi wa Sall unatarajiwa kurejesha hali ya kawaida nchini humo.

 

Website | + posts

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here