Home Kimataifa Machogu: Siombolezi KCPE

Machogu: Siombolezi KCPE

0
kra

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu amesema kwamba haombolezi mwisho wa mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE bali anafurahia kuwa kiungo muhimu wakati ambapo mfumo wa kupima weledi wa wanafunzi unabadilika kutoka KCPE hadi KPSEA.

Alikuwa akizungumza katika afisi za baraza la mitihani nchini KNEC wakati wa kutoa matokeo ya mtihani wa mwisho wa KCPE nchini.

kra

Alifungua hotuba yake kwa njia ya kipekee ambapo alitaja aliyekuwa waziri wa elimu mtihani wa KCPE ulipoanzishwa mwaka 1985, waziri Oloo Aringo.

Kulingana naye Aringo hangejua kwamba mtihani huo ungeendelea kwa miaka 39 na sasa yeye anafurahia kupata fursa ya kutangaza mwisho wake.

Alisifia mfumo wa elimu wa 8.4.4 akisema kwamba ulizalisha wasomi na wataalamu wa kupigiwa mfano ndani na nje ya nchi.

Waziri Machogu alitetea mfumo mpya wa elimu nchini CBC akisema walioutunga na kusaidia katika utekelezaji wake walipitia mfumo unaoondoka wa 8.4.4.