Home Habari Kuu Machogu: Fedha za wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kiufundi kutolewa wiki...

Machogu: Fedha za wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kiufundi kutolewa wiki ijayo

0

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu sasa anasema Bodi ya Kutoa Mikopo ya Elimu ya Juu, HELB imemaliza mchakato wa utayarishaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kiufundi, TVET. 

Machogu anasema fedha hizo zinazotolewa chini ya mfumo mpya wa ufadhili wa elimu ya juu zitaanza kutolewa kwa wanafunzi Jumanne wiki ijayo.

“Kutokana na hilo, Wizara ingependa kuwataarifu wanafunzi ambao maombi yao yalikubaliwa kwamba fedha zitatumwa kwa vyuo vyao husika na akaunti za wanafunzi kuanzia Jumanne, Julai 7, 2023,” alisema Machogu katika taarifa fupi leo Ijumaa.

“Wanafunzi wanashauriwa kuhakikisha maelezo yao ya benki, kama yalivyoelezwa katika fomu za kutuma maombi ya mikopo ni sahihi.”

Hatua hiyo inakuja wakati ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wamekuwa wakilalamikia ukawishwaji wa fedha hizo wanazosema umefanya maisha kuwa magumu na kutishia wao kuzuiwa kufanya mitihani.

 

Website | + posts