Home Kimataifa Machafuko baada ya uchaguzi yachacha visiwani Comoros

Machafuko baada ya uchaguzi yachacha visiwani Comoros

0

Hali ya taharuki ingali imetanda visiwani Komoro baada ya upinzani kukataa matokeo ya uchjaguzi wa Urais .

Kulizuka makabiliano makali baina ya wanadamanaji wa upinzani na maafisa wa polisi katika barabara za mji mkuu Moroni, huku watu kadhaa wakiripotiwa kujeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Polisi waliwafyatuliwa waandamanaji vitoa machozi katika makabiliano hayo yaliyoanza siku mbili, baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Urais ambapo Azali Assoumani alitangazwa mshindi.

Website | + posts