Home Michezo Mabinti wa Kenya waangukia pua Cameroon

Mabinti wa Kenya waangukia pua Cameroon

0

Timu ya Kenya kwa wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 almaarufu Rising Starlets, iliambulia kichapo cha mabao matatu kwa nunge ugenini dhidi ya Cameroon katika mkumbo wa kwanza raundi ya tatu, kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao.

Rising Starlets walipigwa magoli yote katika kipindi cha kwanza kwenye mchuano huo wa Jumamosi jioni katika uga wa Ahmadou Ahidjo mjini Younde.

Matokeo hayo yametia doa harakati za vipusa hao wanaonolewa na kocha Beldine Odemba, kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Colombia, kwani wanahitaji ushindi wa magoli manne kwa bila jijini Nairobi ili kuingia raundi ya nne.

Mchuano wa marudio utasakatwa Nairobi wiki ijayo.

Website | + posts