Home Michezo Mabingwa watetezi Marekani wafuzu raundi ya 16 ya Kombe la Dunia wakichechemea

Mabingwa watetezi Marekani wafuzu raundi ya 16 ya Kombe la Dunia wakichechemea

Michuano ya makundi itakamilika Jumatano kabla ya mapumziko ya siku mbili na kisha kupisha mechi za raundi ya 16 bora kuanzia Jumamosi

0
kra

Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Marekani wamejikatia tiketi ya raundi ya 16 bora ya mashindano ya Kombe la Dunia kwa wanawake, licha ya kutoka sare tasa na limbukeni Ureno katika mchuano wa kundi E uliopigwa mapema leo Jumanne, uwanjani Eden Park mjini Auckland New Zealand.

Katika matokeo mengine ya kundi hilo, Uholanzi wameichakaza Vietnam mabao 7 kwa nunge na kuliongoza kwa alama 7 wakifuatwa na Marekani kwa alama 5.

kra

Mataifa yaliyofuzu kwa raundi ya 16 bora kufikia sasa ni Uswizi na Norway katika kundi A, Australia na Nigeria kutoka kundi B, Japani na Uhispania kutoka kundi C, na Uholanzi na Marekani za kundi E.

Michuano ya makundi itakamilika kesho Jumatano kabla ya mapumziko ya siku mbili na kisha kupisha mechi za raundi ya 16 bora kuanzia Jumamosi wiki hii ambapo Uswizi watacheza dhidi ya Uhispania nao Japani wapimane nguvu na Norway.

Website | + posts