Mabingwa watetezi Argentina na Canada wamefuzu kwa robo fainali ya kipute cha COPA America kinachoendelea nchini Marekani,baada ya kusajili ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Peru katika mechi ya tatu ya kundi A mapema Jumapili.
Argentina waliongoza kundi hilo kwa tisa kutoka wakifuatwa kwa umbali na Canada kwa alama 4, baada ya kutoka sare tasa na Chile mapema Jumapili.
Chile na Peru wamebanduliwa mashindanoni.
Mechi za kundi B zitakamilika mapema Jumatatu, Ecuador itachuana na Mexico Kundini B ,wakati Jamaica ikimaliza udhia na Venezuela.
Venezuela wamo kileleni kwa alama sita wakifuatwa na Ecuador na Mexico kwa pointi 3 kila moja nao Jamaica hawana pointi.