Home Michezo Mabarubaru Wanyonyi na Kipng’etich kuwania tiketi ya fainali ya mita 800

Mabarubaru Wanyonyi na Kipng’etich kuwania tiketi ya fainali ya mita 800

0
EUGENE, OREGON - JULY 23: Emmanuel Wanyonyi of Team Kenya competes in the Men's 800m Final on day nine of the World Athletics Championships Oregon22 at Hayward Field on July 23, 2022 in Eugene, Oregon. (Photo by Carmen Mandato/Getty Images)

Chipikuzi wa Kenya Emmanuel Wanyonyi na Alex Kipng’etich watajitosa uwanjani Alahamisi usiku mjini Budapest,Hungary kwenye fainali ya mita 800 huku mashindano ya Riadha Duniani yakiingia siku ya 6.

Kipng’eticha aliye na umri wa miaka 23 ni mshindi wa nishani ya fedha ya dunia kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 20,na pia ni bingwa wa Afrika katika kitengo hicho na atakuwa katika mchujo wa .

Wanyonyi ambaye ni bingwa wa dunia kwa chipukizi  walio chini ya umri miaka 20 amekuwa na msimu wa kufana ambapo ameshinda mbio za diamond league katika mikondo ya Paris na Rabat na kushinda mbio za Inter continental tour mikondo ya Ostrava na Kip Keino Classic, kabla ya kushinda majaribio ya kitaifa uwanjani Nyayo.

Wanyonyi atalenga kufuzu kwa fainali na kuwania medali baada ya kumaliza wa nne mwaka uliopita nchini Marekani.

Kenya hadi sasa imezoa medali tatu,dhahabu moja ,fedha moja na shaba moja.

Marekani inaongoza kwa nsihani 14 dhahabu 7 fedha 4 na shaba 3,ikifuatwa na Uhispania kwa dhahabu 4  huku Uingereza ikishikilia nafasi ya tatu kwa dhahabu 2 fedha 1 na shaba 1.