Home Habari Kuu Mabanati wa Kenya wanusa Kombe la Dunia baada ya kuizabua Burundi

Mabanati wa Kenya wanusa Kombe la Dunia baada ya kuizabua Burundi

0

Vidosho wa Kenya wanakaribia kuandikisha historia kuwa timu ya kwanza ya Kenya, kufuzu kwa fainali za kombe la dunia chini ya umri wa miaka 17, baada ya kuicharaza Burundi mabao 3-0.

Mechi hiyo ya duru ya kwanza raundi ya nne imesakatwa Jumapili alasiri uwanjani Abebe Bikila mjini Adis Ababa,Ethiopia.

Lorna Faith na Marion Serenge walitikisa nyavu kunako dakika ya 11 na 43, mtawalia huku Kenya wakiongoza mawili kwa bila kufikia mapumzikoni.

Susan Akoth alihitimisha kibarua kwa Starlets katika dakika ya 71 na Kenya wanahitaji sare au hata kushindwa mabao 2-0 katika mechi ya marudio Jumapili ijayo, ili kufuzu kwa fainali za kombe la dunia.

Kipute cha kombe la dunia kutaandaliwa katika Jamhuri ya Dominika Novemba mwaka huu.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here