Home Michezo Mabanati wa Kenya waimarisha mazoezi kuikabili Burundi

Mabanati wa Kenya waimarisha mazoezi kuikabili Burundi

0
kra

Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17, imeimarisha mazoezi kwa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Burundi mwishoni mwa juma hili.

Junior Starlets inavyojulikana imefanya mazoezi mapema Jumatatu katika uwanja wa Dandora, kujitayarisha kwa mechi ya raundi ya nne kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia baadaye mwaka huu .

kra

Mkumbo wa kwanza utapigwa Adis Ababa,Ethiopia Juni 9 huku marudio yakipangiwa nchini Kenya tarehe 16 mwezi huu.

Vipusa hao wataondoka nchini Juni 7 kwa mechi ya duru ya kwanza Jumapili hii uwanjani Abebe Bikila.

Mshindi wa jumla baada ya mikondo mwili atajiaktia tiketi kwa fainali za Kombe la Dunia katika Jamhuri ya Dominika,mwezi Oktoba mwaka huu.

Website | + posts