Home Kimataifa Mabadiliko ya tabia nchi: Waziri Duale aipongeza Mandera kwa kushinda tuzo

Mabadiliko ya tabia nchi: Waziri Duale aipongeza Mandera kwa kushinda tuzo

0
kra

Waziri wa Mazingira Aden Duale ameipongeza kaunti ya Mandera kwa kushinda tuzo ya kipengele cha mabadiliko ya tabia nchi ya Living Green. 

Kaunti hiyo ilishinda tuzo hiyo kwenye Kongamano la Future Green City, 2024 lililofanyika mjini Utrecht nchini Uholanzi.

kra

Mpango wa kijani wa manispaa ya Mandera uliibuka kidedea katika kipengele chake kwenye dhifa ya tuzo za dunia iliyoandaliwa na Chama cha Kimataifa cha Wazalishaji wa Kilimo cha Bustani (IAHP) Septemba 25, 2024.

Mji wa China wa Chengdu ulishinda tuzo Kuu ya Jumla wakati wa hafla hiyo kutokana na mpango wake wa Urban Green Heart Programme.

Washindi wengine katika mashindano hayo yaliyokuwa na vipengele saba walikuwa miji ya Sao Paulo (Brazil), Joondalup (Australia), Mexico City (Mexico), Baia Mare (Romania) na Curitiba (Brazil).

Septemba 2024 kwenye afisi yake jijini Nairobi, Duale aliuaga ujumbe wa kaunti ya Mandera ulioenda kushiriki mashindano hayo wakati wa mkutano uliohudhuriwa na Gavana wa Mandera Mohamed Adan Khalif.

KBC Digital
+ posts