Home Habari Kuu Mabadiliko ya Tabia Nchi: Mchungaji Dorcas aitaka Afrika kuzungumza kwa sauti moja

Mabadiliko ya Tabia Nchi: Mchungaji Dorcas aitaka Afrika kuzungumza kwa sauti moja

0

Mke wa Naibu Rais Dorcas Rigathi amesema nchi hii iko katika mstari wa mbele katika kufanya maamuzi yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza wakati wa Kongamano linaloendelea la Afrika kuhusu Tabia Nchi katika jumba la KICC, Mchungaji Dorcas amesema ni wakati wa Afrika kuzungumza kwa sauti moja na kufanya maamuzi magumu. 

“Afrika inazungumza, Afrika inafanya maamuzi na kuchukua hatua dhidi ya matishio yaliyopo. Kenya imejipata katika mstari wa mbele katika mazungumzo ya dunia juu ya mabadiliko ya tabia nchi. Hii inatoa fursa muhimu ya kushiriki ipasavyo katika mazungumzo haya muhimu.”

Mchungaji Dorcas kadhalika alisema mpango unaoendelea wa upanzi wa miti unapaswa kutumiwa kama fursa ya kubuni nafasi za ajira kwa vijana kote barani Afrika. 

“Tunapaswa kutumia uwezo wa ukuaji kijani kama njia ya kubuni nafasi za ajira na kuhakikisha ustawi wa vizazi vijavyo”.