Home Habari Kuu Maandamano yashuhudiwa Amsterdam baada ya Rais wa Israel kuonekana huko

Maandamano yashuhudiwa Amsterdam baada ya Rais wa Israel kuonekana huko

0
kra

Rais wa Israel Isaac Herzog alihudhuria ufunguzi rasmi wa jumba la makumbusho ya Holocaust jijini Amsterdam nchini Uholanzi hatua iliyosababisha maandamano jijini humo.

Waandamanaji walikuwa wanalalamikia oparesheni za kijeshi za Israel katika ukanda wa Gaza wakati wa ufunguzi rasmi wa jumba hilo Jumapili Machi 10, 2024.

kra

Wanaharakati hao walisikika wakiimba nyimbo za kutaka vita visitishwe katika eneo la Gaza, huku wakiwa wamebeba bendera za Palestina na Israeli.

Baadhi ya waandamanaji waliingia kwenye gari za maafisa wa polisi jijini Amsterdam kulalamikia oparesheni ya Israel huko Gaza ambayo imesababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 31 kulingana na wizara ya Afya ya Palestina.

Israel ilianzisha oparesheni hiyo baada ya kundi la Hamas kutekeleza mashambulizi katika miji kadhaa ya Israel na kuua watu wapatao 1,139 Oktoba 7, 2023.

Polisi jijimi Amsterdam walilazimika kutumia kila mbinu kutawanya waandamanaji hao waliokusanyika nje ya jumba la kitaifa na makumbusho ya mauaji ya halaiki ya Holocaust miaka 80 tangu mwisho wa vita vya pili vya dunia.

Mwaliko wa kuhudhuria ufunguzi wa jumba hilo kwa Rais wa Israeli Isaac Herzog, ulitolewa hata kabla ya uvamizi huo wa Hamas nchini Israel.

Vitu 2,500 vya ukumbusho wa mauaji hayo ambavyo havikuwa vimeonyeshwa kwa umma awali vinaatikana kwenye jumba hilo ambalo sasa linaweza kufikiwa na kila mmoja.