Home Kimataifa Maandamano yaandaliwa jijini London kwa mara nyingine kuhusu mzozo wa Gaza

Maandamano yaandaliwa jijini London kwa mara nyingine kuhusu mzozo wa Gaza

0

Watu wengi waliandamana kwa mara nyingine kwenye barabara za jiji kuu la Uingereza London, wakitaka Israel isitishe mashambulizi yake katika ukanda wa Gaza.

Waandamanaji hao waliinyoshea serikali yao kidole cha lawama pia kwa kukosa kupiga kura kupendelea kusitishwa kwa vita katika ukanda huo.

Walitembea kutoka makutano ya Bank hadi majengo ya bunge Jumamosi wakiwa wamebeba mabango yenye maandishi kama vile, “Sitisha vita sasa hivi:, “Sitisha mauaji ya halaiki” na “Kutoka mtoni hadi baharini Palestina itakuwa huru” kauli mbiu inayotumiwa sana na wapalestina.

Uingereza ilikosa kupiga kura kama mwanachama wa baraza la usalama la umoja wa mataifa ambayo ililenga kukomesha vita vya Gaza, kura iliyoitishwa na Marekani.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres alichochea kura hiyo pia kwa kutumia kifungu nambari 99 cha mkataba wa umoja wa mataifa, kifungu ambacho hakijatumika kwa miaka mingi akisema kwamba watu wa Gaza huenda wakaangamizwa kabisa.

Kulingana na polisi jijini London, maandamano ya jana yalihudhuriwa na watu wapatao elfu 40, na yaliendelea bila visa vingi huku waandamanaji wakifuata maagizo ya polisi.

Hata hivyo waandamanaji 13 walikamatwa kwa makosa yanayohusiana maneno mabaya kwenye mabango yao. Mmoja wa waliokamatwa alikuwa na bango ambalo lilifananisha Israel na Ujerumani ya “Nazi”.

Website | + posts