Hali ya usalama imeimarishwa mjini Kampala nchini Uganda huku wanajeshi wenye silaha wakionekana kuizingira mitaa baada ya vijana kupanga kuandamana hadi kwenye bunge kuwasilisha madai yao, ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa Spika.
Awali, Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni aliwaonya waandamanaji kwamba “watakuwa wakicheza na moto” ikiwa wataendelea na mipango ya kuandaa maandamano ya kupinga ufisadi hadi bungeni siku ya Jumanne.
Haya ni baadhi ya madai ya waandamanaji waliyopanga kuyawasilisha bungeni leo:
- Kujiuzulu kwa Annet Among kama Spika wa Uganda
- Kujiuzulu kwa makamishna wanne
- Kupunguzwa kwa idadi ya wabunge
- Mbunge yeyote aliyehusika na kashfa yoyote ya ufisadi lazima ajiuzulu wakati uchunguzi ukiendelea
- Kufanyika kwa ukaguzi wa mali na mtindo wa maisha wa wabunge na kuutangaza
- Kukatwa kwa mishahara na marupurupu ya wabunge wote hadi shilingi milioni 3 za Uganda
- Kuwaruhusu Waganda kuendelea kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kukusanyinyika kwa amani bila kizuizi.