Home Taifa Azimio kufanya maandamano siku tatu mtawalia wiki ijayo, adokeza Seneta Sifuna

Azimio kufanya maandamano siku tatu mtawalia wiki ijayo, adokeza Seneta Sifuna

Sifuna amefuchua kuwa maandamano hayo yamechochewa na hali ya Rais Ruto kutosikiza malalamishinya Wakenya kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha nchini.

0

Seneta wa kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna amedokeza kuwa maandamano ya upinzani yatafanyika kwa siku tatu mtawalia wiki ijayo.

Maandamano hayo yatafanyika kuanzia Jumatatu hadi Jumatano.

Muungano wa Azimio umekuwa ukifanya maandamano kila siku ya Jumatano, maandamano ambayo yamesababisha vifo vya zaidi watu kumi kufikia sasa.

Makumi ya wengine wameachwa wakiuguza majeraha.

Seneta Sifuna amefichua kuwa maandamano hayo yamechochewa na hali ya Rais William Ruto kutosikiza malalamishi ya Wakenya kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha.

Sifuna ameapa kuwa muungano huo hautalegeza kamba hadi matakwa yao yasikizwe.

Maandano ya jana Jumatano katika kaunti mbalimbali nchini yalisababisha maafa na uharibifu mkubwa, hatua ambayo imelaaniwa vikali na utawala wa Kenya Kwanza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here