Home Kaunti Maambukizi ya kifua kikuu yaongezeka Pokot Magharibi

Maambukizi ya kifua kikuu yaongezeka Pokot Magharibi

Kaunti hiyo iliandikisha wagonjwa 1,617 wa kifua kikuu mwaka wa 2023, huku 220 kati yao wakiwa watoto.

0
Hospitali ya Rufaa ya Kapenguria, Pokot Magharibi.

Waziri wa Afya na Mazingira wa Kaunti ya Pokot Magharibi Paul Woyakapel amesikitikia idadi kubwa ya maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu, TB, akisema yamesababisha vifo vya watu wengi.

Kwa mujibu wa Woyakapel, kaunti hiyo iliandikisha wagonjwa 1,617 wa kifua kikuu mwaka wa 2023 huku 220 kati yao wakiwa watoto.

Aidha, alifichua kuwa magereza ya mgodi wa Rimis na Kanyerus ya Pokot Kaskazini, Cheptuya ya Pokot Magharibi na Kambi Karaya ya Pokot ya kati, yana idadi kubwa ya maambukizi ya ugonjwa huo hatari.

Kwa upande wake, afisa mkuu wa kaunti hiyo Nelly Soprin alisema kuwa mpango wa uhamasishaji unaendelea kwa lengo la kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.

Nelly aliwataka wakazi wa kaunti hiyo walio na dalili za kukohoa, kutokwa na jasho na kupoteza uzani kutembelea vituo vya afya kwa uchunguzi na ikiwa watagunduliwa kuwa na ugonjwa huo, wapokee matibabu.